ZIJUE FAIDA ZA ASALI
Asali imekuwepo toka enzi za
mababu zetu lakini watu bado hawajaelewa umuhimu wa kutumia asali, hasa Asali
Halisi (Asali Mbichi). Watu wengi wamekuwa wakipata shida za kiafya kutokana na
matumizi mabaya ya vyakula, ikiwemo uvIvu wa kufanya mazoezi. Asali ni mkombozi
wa matatizo mengi ya kiafya yanayomsumbua mwanadamu;
Wataalamu wa afya waliofanya
utafiti kuhusu asali na uwezo wa kupunguza unene walibaini kwamba, muda wa saa
nne za mwanzo za usingizi, asali itayeyusha mafuta mengi mwilini sawa na
kufanya mazoezi makali. Tumia asali vijiko 2 vya chai kila unapokwenda kulala,
ni vizuri zaidi tiba hii ikaambatana na kufanya mazoezi kiasi. Umuhimu wa asali
kwenye tatizo la unene ni uwezo wake wa kuyeyusha mafuta mwilini kwa haraka
ukiwa umelala na wakati huo huo kuupa mwili nguvu. Hii ni kwa tatizo la unene,
lakini unaweza kutumia asali kwa matumizi mengine.
ASALI MBICHI(ASALI
HALISI), ZAO LA TANZANIA
Eben-Ezery Mende kwenye Jambo Leo,
Jumamosi ya tarehe 11 Mwezi wa Tano, 2013 aliweza
kueleza mambo mengi kuhusiana na umuhimu wa Asali na hasa Asali Mbichi;
Unaweza kutumia asali na
mdalasini kwa kuchanganya, umoja huo umebainika kusaidia kupunguza uzito.
Mchanganyiko huo unatakiwa uwe wa asali na unga wa mdalasini. Baada ya
kuchanganya vizuri asali na mdalasini Utapata kinywaji kama ilivyo vinywaji
vingine ambapo utatakiwa kuchanganya asali, mdalasini na maji ya moto.
Ukivichanganya vitu hivyo ni
tayari kwa matumizi na hapo unapaswa kunywa mara mbili kwa siku. Chukua nusu
kijiko cha unga wa mdalasini (kijiko kidogo cha chai) kijiko kimoja cha
asali na kikombe kimoja cha maji yaliyochemka.
Hatua ya kwanza ni kuchanganya
maji moto na unga wa mdalasini, koroga hadi uchanganyike vizuri kisha funika na
uache muda wa nusu saa ili maji yapoe. Baada ya maji kupoa, weka asali kijiko
kimoja kisha koroga tena hadi mchanganyiko uwe kama kinywaji.
Asilimia 98 ya watu duniani
wanafahamu vema kwamba mojawapo ya silaha ya ajabu katika kupigana na magonjwa
na matatizo yatokanayo na uzee ni kwa kutumia asali.
Utafiti mpya umeonesha uwezo wa
asali huongezeka maradufu ikichanganywa na mdalasini katika kutatua tatizo la
uzito na kumfanya mtu kuwa na uwezo mkubwa wa fikra na kumbukumbu.
Uchunguzi ufanywao na Jarida la
World News uliohusu tiba, wataalamu wa dawa zitokanazo na mimea na kijarida cha
afya na lishe, imeonekana kuna umuhimu wa asali na mdalasini kwakuwa
mchanganyiko huo ni dawa ya kusisimua iletayo afya bora.
Pia asali inatatua tatizo la
ugonjwa wa viungo na uvimbe ambapo wataalamu wa lishe wanapendekeza kutumia
mchanganyiko wa sehemu moja ya asali na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko
kimoja cha chai chenye mdalasini na kuchua sehemu zilizohathirika.
Tiba hiyo inaanza kuonesha
matunda yake kwa kupata nafuu dakika moja baada ya kutumiwa.
Kama hiyo hutaimudu unashauriwa
kutengeneza chai kikombe kimoja chenye maji ya moto, weka vijiko vya chakula
viwili vya asali kwa kijiko cha chai cha mdalasini kisha unywe asubuhi na jioni
ili kuondoa maumivu.
Utafiti uliofanyika hivi karibuni
na Chuo Kikuu Copenhagen, madaktari waliwapa wagonjwa 200, syrup mchanganyiko
wa kijiko kimoja cha chai cha asali na kimoja cha mdalasini kila asubuhi kabla
ya kifungua kinywa walipata ahueni.
Hata hivyo imebainika kwamba
asilimia 73 ya walioripotiwa kupata ahueni kubwa ya maumivu na ongezeko katika
kufanya shughuli kama kujongea na kutembea vema.
Mbali ya faida nilizozieleza
awali pia katika urembo asali hutumika na hapa unaweza kuitumia kwa kulinda
kukatika kwa nywele.
Asali ikishachanganywa na
mdalasini na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa kichocheo cha kuotesha nywele
kinachotumika katika dawa ya Dork. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa
kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.
Tiba nyingine inayotokana na
asali ni ukungu wa miguuni ambapo unatakiwa kuchanganya kijiko kikubwa cha
mezani cha asali, vijiko viwili vya mdalasini. Paka sehemu zilizoathirika usiku
kwa muda wa nusu saa, kisha safisha kwa sabuni na maji. Tatizo litakwisha baada
ya wiki moja.
Hili nalo ni kubwa ambalo asali
hutumika kulitibu ambalo ni maambukizi kwenye kibofu cha mkojo.
Chukua glasi ya maji vuguvugu
yaliyochanganywa na vijiko viwili vya chai vya mdalasini na kijiko kimoja cha
chai cha asali huondoa bakteria kwenye kibofu. Pia unaweza ukatumia juisi ya
cranberry badala ya maji ikiwa ambukizo la kibofu litakuwa sugu.
Mtu mwenye maumivu ya jino
anaweza kuchanganya sehemu tano za asali na sehemu moja ya mdalasini na tumia
kwa maumivu ya jino kwa kudondoshea kwenye jino au meno yaliyoathirika hadi
maumivu yatakapotoweka.
Saladi ya kupaka vidonda
iliyochanganywa na asali na mdalasini kwenye chai ya raspberry nyekundu ni dawa
nzuri ya kuondoa maumivu makali ya vidonda vitokanavyo na kulala muda mrefu.
Hizo ni baadhi tu ya faida za
asali lakini kila tatizo katika mwili wa binadamu lina nafasi ya kutumia asali
kwa kuchanganya chakula au kimiminika
kingine na mgonjwa akapona kabisa ugonjwa unaomsumbua.
Mwandishi wa safu hii si daktari
wala muuguzi bali yanayoandikwa yanatokana na tafiti, vyanzo vya habari kwa
ushirikianao na wataalamu wa afya ya binadamu.
Ukihitaji Asali Mbichi (Asali Halisi), waweza kutupata,
You Can Find Us,
Mayfair
Plaza-Central Building,
Mwai Kibaki Road,
Dar es Salaam –
Tanzania.
Cell : +255 767 510
564 / 688 510 564
Email :
recafotz@gmail.com.
Blog :
PureNaturalHoney-AsaliHalisi.blogspot.com
Nyuki ni Tabibu wa kwanza hapa duniani, maana Mungu alimfanya hivyo ili wanadamu tufaidi matunda yake. Madaktari wanaweza kutengeneza dawa, vyakula na mambo mengi, lakini sio kama afanyavyo mdudu huyu mwenye uwenzo mkubwa wa kitabibu. Anatengeneza asali ambayo inaweza tumika kama: chakula, kinywaji, dawa, kipodozi au kiungo. Magonjwa karibia yote huweza kutibika kwa mazao ya mdudu huyu nyuki. Jamani nyuki ni kiumbe aliye barikiwa na Mungu. Tumia Asali Mbichi kwa afya ya familia yako.
ReplyDelete